DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, September 22, 2013

Dogo Janja; Naizimia A-Town

 
Msanii wa michano mwenye umri mdogo na kipaji kikubwa hapa Tanzania, Dogo Janja ambaye anaendelea kuwakilisha muziki wake akiwa chini ya usimamizi wa Mtanashati Entertainment, ameweka wazi kupitia eNewz kuhusiana na upendo na mahusiano ambayo ameendelea kuwa nayo na Arusha ambayo ndiyo asili yake, na hii ni katika kuendelea kufuta uvumi kuwa Dar es Salaam imembadilisha na kumsahaulisha alipotokea.

Msanii huyu ambaye anatamba na ngoma yake mpya ya Serebuka, kupitia mahojiano yake na eNewz, ameweka wazi kuwa hawezi kusahau alipotokea na hasa hasa wasanii ambao wana mchango mkubwa katika kumfikisha hapa alipo hususan Nigga C kutoka Jambo Squad.

Dogo Janja amekiri kuwa, Nigga C ni moja kati ya watu ambao wamemfundisha kuandika mistari, pia amekuwa mtu wake wa karibu katika maisha ya kawaida mtaani na kwa kauli yake mwenyewe, Arusha na masela wake wa karibu akiwepo Nigga C ambaye pia ni msanii, ni watu ambao hawezi kuwadiss mpaka mwisho wa maisha.

No comments: