
Msanii wa Bongofleva Snura maarufu kama Majanga, ameweka wazi mipango yake ya kufyatua albam yake hivi karibuni, ambapo amesema amebakiza nyimbo chache tu kuikamilisha.
Hatua ya Snura kujipanga kutoa albam inakuja wakati huu ambapo wasanii wengi wa muziki huu wa kizazi kipya wakiwa na malalamiko makubwa kuwa albam za muziki hazilipi tena.
Pia Snura ambaye nyota yake ilianza kungara kupitia filamu, ameweka wazi mpango wake kuwa hivi sasa atakuwa akitoa filamu kwa kila ngoma ambayo atakuwa akitoa ili kuwapatia burudani sambamba mashabiki wake kwa upande wa filamu na muziki.
No comments:
Post a Comment