
Msanii Dully Sykes ambaye mitaa inasubiri kazi mpya kutoka kwake ambayo inakwenda kwa jina Kabinti Special ambayo ataiachia rasmi ijumaa, tarehe 4/10/2013.
Kazi hii mpya ya Prince Dully Sykes ni inakuja na ladha mpya kabisa, na kwa mujibu wa Dully mwenyewe, Video na Audio ya kazi hii safi, vitaachiwa kwa pamoja ili kutoa ladha kwa ukamilifu kwa mashabiki pande zote.
Dully Sykes pia kwa upande mwingine amesema kuwa, katika kuendeleza kazi zake na kufanya muziki bora zaidi, Yupo katika mchongo wa kuboresha studio yake na amekwishaagiza vifaa vyenye thamani ya zaidi ya dola 20,000 , na hadi sasa vifaa hivi vipo njiani karibia kutua bongo.
No comments:
Post a Comment