DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, September 26, 2013

Olamide agawa 'Mapesa'


 

Msanii wa muziki kutoka nchini Nijeria, Olamide amefanya kitu ambacho kimewashangaza na pia kuwafurahisha wengi, hasa baada ya kuamua kutoa kiasi cha Naira 50,000 ambazo ni zaidi ya shilingi laki 5 za kitanzania, Kwa moja ya shabiki wake aliyemuomba pesa kupitia mtandao wa twitter.

Shabiki huyu mwenye bahati, alipata nafasi hii baada ya kumuomba msanii huyu Naira 10000 kama utani, ambapo msanii huyu alimjibu na kumuomba ampatie namba ya akaunti yake ambapo alitangaza kupandisha dau na kumtoa kitita cha naira 50000.

Kitendo hiki kilichogusa wengi kilipelekea mvua ya maombi mengine ya pesa kwa msanii huyu kutoka kwa mashabiki wengine waliokuwa wakifuatilia tukio hili kwa karibu, lakini maombi yao yaligonga
mwamba kutokana na msanii huyu kuamua kumsaidia mmoja tu.

No comments: