DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Monday, September 16, 2013

HAFSA KAZINJA NA WIMBO WA KUMUENZI MKONGWE MUHIDIN MAALIM GURUMO

Malkia wa Zouk Hafsa Kazinja akiwa na wanamuziki wakongwe Omari Mkali (kushoto) na Abdul Salvador baada ya kumariza kurekodi wimbo wa Muhidin Maalim Gurumo wa “NIMUOKOE NANI” enzi hizo akiwa na NUTA jazz ikiwa ni mchango wake kumuenzi mwanamuziki huyo nguli ambaye amestaafu rasmi muziki baada ya kudumu katika fani tangu mwaka 1960. Hapa ni OM Records jijini Dar es salaam alikorekodia kibao hicho.  

——————————–
Baada ya ukimya wa muda mrefu, Malkia wa Zouk Tanzania, Hafsa Kazinja, anaibuka upya katika fani akiwa na ingizo lake la kwanza kati ya kumi aliyoandaa kwa kuimba wimbo maarufu wa NUTA Jazz Band uitwao “NIMUOKOE NANI” anauouleta hewani katika mahadhi ya Zouk. 
 Hafsa Kazinja anasema ameamua kurudi ulingoni kwa kutoa wimbo huo ili kumuenzi Mzee Muhidin Maalim Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani ya muziki baada ya kufanya kazi hiyo akiwa na bendi mbalimbali tokea mwaka wa 1960. 
 “Nimeamua kuimba wimbo huu wa “NIMUOKOE NANI” ili kumuenzi gwiji huyu wa muziki kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo naibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda”, anasema Hafsa ambaye alitoka kwa wimbo wake wa “PRESHA” aliomshirikisha Banana Zorro. 
 Hafsa ameandaa wimbo huo wa “NIMUOKOE NANI” katika studio za OM Productions ya jijini Dar es salaam chini ya wanamuziki nguli, Abdul Salvador na Omari Mkali.  “Nafurahi kwamba wimbo wa NIMUOKOE NANI nimeuimba baada ya kupata Baraka zote toka kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe.
 “Haikuwa rahisi kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya kwenda kumuona nyumbani kwake alinifanyisha mtihani wa kuuimba wote kabla ya kuridhika maana alisema asingefurahi kuona wimbo wake unaimbwa hovyo hovyo na kuharibiwa radha yake”, anasema Hafsa, ambaye hivi sana anamalizia ngoma zake zingine tisa alizotunga mwenyewe, kabla ya kuvamia anga kwa mara

No comments: