
Kutokana na ngoma zake nyingi kugusia masuala ya dini na siasa, Msanii Bora wa Hip Hop Bongo kwa mwaka huu, Kala Jeremiah amesema kuwa hana wasi wasi kabisa kuhusiana na hofu kuwa aina ya muziki anaoufanya inachangia kuwagawa mashabiki wake.
Kala amesema kuwa yeye ni mtu ambaye anaamini mazuri katika dini zote hasa kutokana na wazazi wake kuwa ni wa imani tofauti tofauti, na pia kwa upande wa siasa Kala amesema kuwa anawasapoti mtu mmoja mmoja kutoka kila chama.
Msanii huyu amesisitiza kuwa hayupo katika chama chochote cha siasa mpaka sasa na kama iinavyofahamika, katika kipindi kifupi kilichopita, msanii huyu aliamua kutangaza waziwazi kuwa anamuunga mkono Mheshimiwa Edward Lowassa kama kiongozi bora na kwa mujibu wake, huyu ndiye kiongozi anayefaa kuwa Rais wa Tanzania, kauli ambayo ilizua mtazamo wa tofauti sana kutoka kwa mashabiki wake.
No comments:
Post a Comment