DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, September 25, 2013

Man Water kuja na mobile studio



 

Katika mpango wa kusaida kukuza muziki wa kitanzania na kupata vipaji vingi zaidi kutoka sehemu mbalimbali Tanzania, Producer wa muziki Man Water kutoka Combination Sound amesema kuwa ana wazo la kuanzisha 'Mobile Studio' ambayo itakuwa inazunguka mikoa mbalimbali na kutoa huduma ya kutengeneza muziki.

Man Water amesema kuwa, Wazo hili limekuja baada ya kuona kuwa kuna vipaji vingi vya muziki kutoka mikoani ambavyo havipati nafasi ya kusikika wala kurekodi kazi zao na wala nafasi ya kusafiri mpaka jijini Dar ambapo huduma hii inapatikana kwa wingi na ubora zaidi.

Man Water amesema kuwa, wazo hili ambalo yupo katika mchakato wa kulishughulikia litazingatia mahitaji yote ya watu ambao analenga kuwafikia, ikiwepo bei chee za kurekodi muziki, na hapa anasema mwenyewe.

No comments: