DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, September 13, 2013

KMT 2013 kuiteka Dar



Tamasha la Muziki la Kili Music Tour 2013 linatarajiwa kumalizika kwa kishindo jumamosi hii katika uwanja wa leaders club kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kufanya vyema katika mokoa kadhaa ya Tanzania.
 
Wajanja wote na wapenzi wa burudani jiji la Dar es Salaam tunakutana kesho jumamosi pale Leaders Club ambapo tutafurahia pamoja muziki wa kikwetu kwetu kwa Live Perfomances kutoka kwa wasanii Fid Q, Roma, Izzo Business, Ney wa Mitego, Madee, Mzee Yusuph, Kalajeremiah, Lady Jaydee, Linex, Ben Pol, Professa Jay, Joh Makini, Mashujaa Band na Diamond.
 
Ni bonge moja la lineup ambalo mchongo wake unaanza jioni flani hivi, unalipa mlangoni shilingi 2500, inafaidishwa na bia moja ya Buree mlangoni, alafu unadondoshewa burudani ambayo utabaki unaisimulia kila siku katika maisha yako.

No comments: