
Kundi maarufu la muziki nchini Kenya Sauti
Sol linatarajiwa kukonga nyoyo za mashabiki katika tamasha kubwa
lililobatizwa jina ‘Lake of Stars
Festival’ litakalofanyika tarehe 27 na 28 mwezi huu nchini Malawi.
Bendi hiyo imealikwa katika project kubwa ambayo itakuwa inafanya
sherehe za kumbukumbu ya miaka 10 ya uanzilishi wa kituo cha sanaa za
muziki, filamu, maigizo, maonyesho mbalimbali yanayohusiana na
kuutangaza utamaduni wa nchi hiyo duniani.
Aidha, tamasha hilo litasheheni wasanii na makundi mbalimbali
barani Afrika wakiwemo Yadi, George the Poet, Sauti Sol, Tumi,Yolanda
Kaluma, na wengineo wengi.
No comments:
Post a Comment