DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!
MAMA MANGWEA: MwanaFA ALITIMIZA AHADI
Mama wa MwanaHip Hop aliyewahi kuaminika kuwa bingwa wa
mitindo huru, Albert Mangwea aliyefariki mwezi Mei mwaka huu, Denisia
Costantine Mangwea ameibuka na kumtetea mwanamuziki wa kizazi kipya
Hamis Mwin’juma ambaye anatuhumiwa kuahidi pesa kwa mama huyo na kuingia
mitini.
Sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa tangu mwishoni
mwa wiki iliyopita, linatokana na kitendo cha mwanamuziki huyo (MwanaFA)
ambaye aliwahi kuahirisha onesho lake, baada ya kifo cha msanii
mwenzake (Albert Mangwea), kutokuweka hadharani hitimisho la ahadi
aliyoitoa kwa familia ya marehemu.
No comments:
Post a Comment