DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, September 22, 2013

Masogange aachiwa kwa dhamana

 

Mtanzania aliyeibukia katika kupamba video za muziki Agness Masogange na mwenzake Melisa Edward waliokamatwa kwa kutuhumiwa kubeba dawa za kulevya nchini Afrika Kusini wameachiwa kwa dhamana.

Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Kulevya Afrika Kusini, Kamishna Toto Mangaleni amethibitisha kuwa watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana, lakini wataendelea kubaki Afrika Kusini wakati kesi yao ikiendelea.

Mangaleni amesema wanawake hao ambao juzi pia walipanda kizimbani, walipata dhamana hiyo jana kutoka Mahakama Kuu ya Gauteng iliyoko eneo la Kempton Park Jijini Johannesburg.

No comments: