DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, September 22, 2013

H Baba ajimwagia masifa

 

Msanii wa muziki ambaye anajinadi na kujivunia sifa ya kuwa msanii anayeongoza kwa ujuzi wa kutumbuiza jukwaani hapa Bongo, H Baba ama baba Tanzanite ametoa ujumbe mzito kwa wasanii wenzake ambao kwa mujibu wake, bado hawana uwezo wa kutumbuiza jukwaani kama alionao yeye.

H Baba ametoa dongo kuwa, wasanii wengine bongo wanategemea madansa ili kupendezesha showz zao jukwaani tofauti na yeye ambaye amejitaja kama proffesional dancer, na amewaonya kuwa wajipange ili kufikia kiwango chake kwasababu jukwaa sio TV.

H Baba ameongeza kuwa, ingawa yeye pia anatumia madansa katika kufanya maonyesho, madansa wake wana kitu cha zaidi na cha kipekee kuanzia muonekano mpaka namna wanavyodansi ambapo amewataka wasanii wengine kujifunza kutoka kwake.

Kwa sasa wachambuzi wa mambo bado wanasubiri kuona kama kuna majibu ama mawazo ya tofauti yoyote kutoka kwa wasanii wengine kuhusiana na maoni ama kile ambacho amekisema H Baba.

No comments: