
Ile kolabo ya mwaka inayomhusisha msanii wa Uganda, Navio pamoja na msanii wa kimataifa Keith Sweat tayari imeshaanza kuwa gumzo mtaani hasa kutokana na uwezo na uzoefu na muunganiko wa wasanii hawea wawili ambao wana heshima za kipekee katika aina za muziki wanaoufanya.
Kolabo hii inakwenda kwa jina On and On na imefanyika huko Atlanta
Marekani katika studio binafsi ya msanii Keith Sweat, na habari mpya
kutokana na mpango huu ni kuwa, mipango ya video ya kazi hii tayari
imeanza kufanyika ambapo hivi karibuni Navio anatarajia kurudi Atlanta
kwaajili ya kumalizia kazi hii.
Wimbo huyu umetajwa pia kushughulikiwa na wataalamu wa kufanya
mastering ambao ni wa kimataifa zaidi ili kuleta ladha ambayo
itathibitisha ushiriki wa wakongwe na wasanii wanaoweza na kujua kile
wanachokifanya.
No comments:
Post a Comment