DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, September 13, 2013

Rema ajibu mapigo




Baada ya msanii Rema Namakula kufukuzwa katika kundi la Gagamel na hivi karibuni Bebe Cool ambaye ni Boss wa Gagamel kutambulisha msanii mpya mwenye umri wa miaka 10 kutoka Kongo na kusema kuwa msanii huyu kinda ndiye atakayekuwa kichwa kitakachoziba nafasi ya Rema, Rema mwenyewe ameamua kusimama na kuzungumzia swala hili.
 
Rema ameongea na mashabiki wake na kuwaambia kuwa, katika maisha siku zote wasiwapatie watu wengine nafasi ya kuwadharau na kuwafanya wajione kuwa sio kitu na sambamba na ujumbe huu, msanii huyu amewaomba mashabiki waendelee kumsapoti na kujitokeza kwenye showz zake.
 
Rema amesema haya hasa kutokana na maneno zaidi na ya kuudhi kutoka kwa Bebe Cool kuwa hakumtengeneza msanii kama Rema kwaajili ya kutumbuiza katika maonyesho madogo zikiwepo sherehe za Harusi, bali alimtengeneza kuwa msanii wa ngazi ya maonyesho makubwa ya kimataifa.

No comments: