DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!
Friday, September 6, 2013
Chameleone kukinukisha Malawi
Siku ya leo itakuwa na shangwe nchini Malawi, hasa kutokana na uwepo wa wasanii Jose Chameleone pamoja na AK47 ambaye ni mdogo wake wa damu, ambao wanatarajia kufanya bonge moja ya onyesho nchini humo. Onyesho hili ambalo litafanyika katika Jiji la Lilongwe, linatarajiwa kuwa ni la aina yake, na tayari wasanii hawa wawili wapo nchini huko, na baada ya onyesho hili, Chameleone ataelekea UK kwa ajili ya kutumbuiza katika mkutano wa Uganda Convention UK mwaka 2013. Chameleone pamoja na mdogo wake watafanya maonyesho siku ya jumamosi na jumapili pia kabla ya kuondoka nchini humo na kuendelea na ratiba nyingine za shughuli zao za kimuziki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment