DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!
Friday, September 6, 2013
P-Unit wakubalika Marekani
Kundi la muziki la P Unit ambalo kwa sasa lipo ziarani huko Marekani, limekuwa na wakati mzuri hasa kutokana na kupata mashabiki wengi katika maonyesho yao ambayo mpaka sasa wameshakamilisha katika miji mikubwa kabisa huko Baltimore, Houston, Atlanta, Dallas na Los Angeles.
Kwa sasa bado ziara ya maonyesho yao zinaendelea ambapo wakali hawa wamebakiza maonyesho kadhaa ambayo watafanya huko Kansas, Minnesota na Boston ambapo wana-Afrika Mashariki hususan wakenya wanaoishi huko wameonyesha msisimko mkubwa na mapokeo mazuri kwa kundi hili tangu mwanzo.
P Unit wanatarajiwa kurudi Kenya katikati ya mwezi huu kabla ya kujiandaa tena kwenda Dubai kwa ajili ya ratiba za maonyesho mengine, hii ikiwa ni ishara tosha ya namna kundi hili linavyokubalika nje ya mipaka ya Kenya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment