DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, October 29, 2013

Bella asema sasa amekuwa

 

Baada ya msanii nyota wa muziki wa dansi Christian Bella kuchukua hatua ya kuanzisha kundi lake mwenyewe la muziki ambalo amelipatia jina Malaika, msanii huyu amefafanua sababu ya yeye kuamua kutoka katika bendi ya Akudo Impact ambayo amekuwa akifanya nayo kazi miaka ya nyuma kabla ya kuelekea huko Sweden ambapo amekuwepo kwa takriban mwaka kabla ya kurejea nchini Tanzania.

Christian Bella amesema kuwa hajaacha kufanya muziki na Akudo kwa maelewano mabaya ila hii ni hatua yake ya kujaribu kufanya kitu chake mwenyewe baada ya kukua na kukomaa kimuziki, kama vile inavyokuwa mtoto akikuwa na kutoka kwa baba na mama na kuanza kujitegemea.

Msanii huyu pia amezungumzia ujio wa kundi lake hili jipya la Malaika ambalo kazi zake zimeanza kushambulia kwa kasi vituo mbalimbali vya radio na televisheni ambapo amesema kuwa tarehe 15 mwezi ujao, anatarajia kufanya onyeshio kubwa jijini Dar es Salaam kutambulisha onyesho hili.

No comments: