DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, October 29, 2013

Madraxx aicharukia Naija Nite


 

Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Madtraxx amepatwa maswahibu makubwa hada baada ya kuzuiliwa kufanya shoo katika onyesho kubwa la Naija Nite huko Nairobi kama ilivyokuwa imetangazwa, kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kugeukwa na waandaaji wa onyesho hilo katika dakika za mwisho kabisa.

Kwa mujibu wa Madtraxx mwenyewe, waandaaji wa tamasha hili waliamua kumtumia yeye na jina lake kwa ajili ya kuongeza nguvu na kuvutia watu wengi zaidi, na kitendo cha yeye kushindwa kufanya onyesho kimemuudhi yeye binafsi pamoja na mashabiki wake, kitu ambacho si sahihi kabisa.

Msanii huyu kwa mujibu wa taarifa, kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya kufungua mashtaka na kudai fidia kwa waandaaji wa Naija Nite kwa kutumia jina lake kujitengenezea faida kinyume cha sheria.

No comments: