
Msanii D Banj kutoka Nigeria, anatarajia kupambana jukwaani pamona na msanii Bebe Cool kutoka Uganda katika tamasha kubwa kabisa la The Battle of The Titans ambalo litafanyika huko Zimbambe tarehe 26 mwezi huu.
Tamasha hili kubwa kabisa Afrika pia litawakutanisha wasanii wengine wakali kupimana uwezo jukwaani, na mpambano huu kati ya D Banj na Bebe Cool unatarajiwa kuwa na aina yake hasa kutokana na mvuto wa wasanii hawa pamoja na idadi kubwa ya mashabiki ambao wanao huko Zimbabwe.
Tayari mpaka sasa mipango yote imeshawekwa sawa kwa ajili ya Tamasha hili ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenda burudani kutoka Kusini na Afrika ya Kati.
No comments:
Post a Comment