DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, October 24, 2013

Selekta kuwangarisha wanamichano

 



Prodyuza anayeshikilia tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki anayechipukia kwa mwaka 2013 Mesen Selekta, wa De'Fatality Music ameanzisha harakati za kunyanyua zaidi muziki wa Hip Hop pamoja na kuonyesha uwezo wa wasanii kwenye kughani mashahiri kupitia mpango alioanzisha unaofahamika kama The Black Gifted Cypher.

Kwa mujibu wa waratibu wa mpango huu pamoja na mtayarishaji muziki Mesen Selekta ambaye ndiye atakuwa akihusika na kusuka midundo ya kazi hizi, Black Gifted Cypher itakuwa inatoka kwa awamu na kushirikisha wasanii 7 kila toleo,  na tayari awamu ya kwanza imekwishaanza kufanyika chini ya studio za De'fatality na kushirikisha wasanii Climax Bibo, P Bling, Tash na wengineo.

Mesen amesema kuwa ili kuwasaidia wasanii wenye uwezo na waliokosa nafasi ya kusikika, Gifted Black Cypher itahusisha wasanuii wenye majina makubwa wa Hip Hop pamoja na wale wachanga na kila baada ya wiki mbili toleo la Cypher hii litakuwa linaingia mtaani kwa njia ya mtandao na televisheni pia.

No comments: