
Wasanii wanaounda kundi la Kimya Band nchini Tanzania wakiwemo Dar 79, Easy G na Macho Kazi wameelezea kuwa pamoja na muziki kuchukua sehemu kubwa katika kazi zao wameamua pia kuendeleza fani zao kwa kuchukua mafunzo ya ufundi wa ndege na uhandisi katika Chuo kimoja Jijini Dar es Salaam.
Akiongea na eNewz mmoja wa memba wa kundi hilo Dar79 amesema kuwa pamoja na kozi yao hiyo hivi sasa wanaendelea kufanya muziki ambapo hivi karibuni wamefyatua kichupa chao kipya ambacho ni singo yao iliyobatizwa jina 'Vicheche Basi' chini ya studio ya Kimya Records.
Aidha, wasanii hao ambao makazi yao ni Yombo pande za Temeke Jijini DSM wamekwishatoa kazi zao mbalimbali ikiwemo audio albam yao yenye nyimbo 12 wakitangulia na video yakwanza 'Mama Nonino' ikifuatiwa na 'Vicheche Basi' iliyotambulishwa kwa mara ya kwanza hapa EATV.
No comments:
Post a Comment