
Msanii Ssen Lubi ambaye kazi yake ya fungu la kukosa kati ya nyinginezo ndiyo iliyomtambulisha poa katika gemu ya muziki Bongo, ametangaza kuwa, moja ya project zake kubwa kabisa kuwahi kufanyika ambayo ni kazi inayokwenda kwa jina Kiroho Safi ambayo amemshirikisha msanii Chegge Chigunda mtoto wa mama Said, imeshakamilika na sasa ipo katika hatua za mwisho za upakiaji kabla ya kuachiwa rasmi.
SSen ambaye mbali na kazi zake za binafsi pia ni back vocalist mkali kabisa wa msanii Linex Sunday, amewahakikishia watanzania kuwa hii ni moja ya kazi kali kabisa za kusubiri kutoka kwake hasa kutokana na maandalizi makubwa ambayo yamefanyika juu yake.
Msanii huyu amesema kuwa, anaamini ataleta mapinduzi na mabadiliko katika muziki kutokana na kuisoma game kwa muda na kujipanga kutoa kitu cha tofauti na chenye mvuto kwa jamii, na hii ni chini ya Seductive Records kwenye mikono safi ya Producer Mr T Touch.
Audio na video za kazi hii zitatoka kwa pamoja ambapo mpango mzima wa Video ya kazi hii umesimamiwa na Director Solomon Lamba wa Emptysouls Productions.
No comments:
Post a Comment