DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, October 24, 2013

Izzo ajipanga kuongeza ubora

 

Rapa Izzo Business, amesema kuwa kutokana na kujipanga sana na pia kuhusisha timu ya watu makini kumshauri juu ya muziki wake, anaamini kabisa kuwa kazi ama projects zake ambazo zitakuwa zinatoka kuanzia sasa na kuendelea zitakuwa hazina mfano wake kutokana na uzuri na ubora ambao utakuwa umehusika ndani yake.

Izzo Business amesema kuwa, kutokana na utaratibu huu anaamini kwa asilimia 100 kuwa kazi ambayo itakuja kutoka kwake hivi karibuni itatingisha taifa kutokana na kujipanga sana linapokuja swala zima la ubora.

Izzo Business amesema kuwa, Kuna umuhimu mkubwa wa hata wasanii wengine kufanya kazi katika kiwango ambacho hata wale wasikilizaji ama watazamaji wa kazi zao, wataweza kutambua na kuona ile nguvu ama akili pamoja na thamani ambayo wamewekeza katika kufanya kazi husika.

No comments: