DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, October 3, 2013

Mzee Sykes: Nitapiga pamba tu


 
Mzee Sykes, ambaye ni msanii mkongwe wa muziki na pia Baba wa msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye anafanya poa sana katika gemu Dully Sykes, amefafanua sababu za yeye kuendeleza muonekano wake wa ujana licha ya kuwa na umri mkubwa tofauti na wazee ama wasanii wengine wanavyojiweka.

Mzee Sykes amesema kuwa, kutokana na nafasi yake kama msanii hajaona sababu ya kujibadilisha na kujiweka katika muonekano na mavazi sawa sawa na umri wake kutonana na mapenzi makubwa aliyonayo katika swala zima la mitindo na kile alichokita yeye 'culture'.

Mzee huyu amesisitiza kuwa hana mpango wa kubadilika kwasababu yeye ni msanii wa muziki ambaye muziki na mitindo ipo katika damu yake.

No comments: