DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, October 3, 2013

Daz Baba; Sijachanganyikiwa

 


Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa msanii wa muziki Daz Baba amechanganyikiwa na mekuwa akionekana mitaani akifanya vitu visivyoeleweka, eNewz imeweza kukutana na msanii huyu katika mitaa ya Yombo Jijini Dar es Salaam na kupata nafasi ya kusikia ufafanuzi wake kuhusiana na taarifa hizi nzito dhidi yake.

Daz Baba ambaye amesema kwa sasa ameamua kurudi shule na kujiendeleza kusoma, kupitia mahojiano tuliyofanya naye, amekanusha vikali taarifa kuwa  amerukwa na akili na kukiri kuwa saa nyingine mtu anaweza kufanya kitu cha ajabu hasa kutokana na 'stress' nyingi ikiwepo kwa yeye bbinafsi kushuhudia watu wa karibu wakipoteza maisha akiwepo marehemu Ngwea, Mark2b na wengine.

Daz amesema kuwa amesikitishwa na taarifa kuchapishwa kuwa amechanganyikiwa bila ya yeye kuulizwa chochote na chombo husika na ameomba vyombo vya habari kuacha kuripoti mambo mabaya kuhusiana na wasanii, na kuweka msisitizo zaidi katika kazi na maendeleo yao.

Daz pia amekanusha taarifa zilizopo mtaani kuwa anatumia Dawa za kulevya na kusema kuwa, yeye hatumii hata sigara na maisha yake yanakwenda sawa sawa.

No comments: