
Rapper huyo alimiminiwa risasi wakati akiwa katika gari lake alipokuwa akitoka Petrol Station kujaza mafuta kwenye gari na ndipo mapolisi walipoanza kushambulia gari lake kwa risasi bila ya kutoa onyo na kumuumiza rapper huyo kwenye mkono wa kulia na mgongoni kwa risasi.
Kisa cha rapper huyo kupigwa risasi hizo, inasemekana kuwa ni kumfananisha rapper huyo na gari lake, na wahalifu ambao walikuwa wakitafutwa na polisi.
Habari kutoka kwa meneja wa rapper Khuli Chana, amesema kuwa rapper huyo alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu haraka na kwamba rapper huyo kwa sasa anaendelea vizuri na ameshapata ruhusa yuko nyumbani kwake anaendelea kuuguza majeraha aliyoyapata katika msukosuko huo.
No comments:
Post a Comment