
Kundi maarufu la muziki Jijini Kigali nchini Rwanda, la Two 4real ambalo hivi sasa lina make headlines Afrika Mashariki limeonyesha nia na furaha yao ya kushirikiana na wasanii wa Afrika Mashariki.
Wakiwa wanafanya vyema na wimbo wao 'Agakayi' kundi hilo limeongea na eNewz kuwa wanamfagilia sana msanii Alikiba kutokana na kuwahi kushirikiana nae katika maswala ya muziki ambapo mambo yakienda powa wanatarajia kufanya nae kolabo.
Aidha, pia wameweka wazi kuwa hivi sasa kuna project yao mpya ya muziki walioshirikisha wasanii wa Uganda wakiwemo Toniks na Ray signature ambapo pia wapo mbioni kupiga kazi na Bebe Cool, Wyre na General Ozzy kutoka Zambia.
No comments:
Post a Comment