
Msanii wa muziki kutoka Kenya, Victoria Kimani ameendelea kupasua mawimbi katika muziki wake, na safari hii ameandika historia mpya baada ya kupata nafasi ya kufanya onyesho katika jukwaa moja na msanii wa kimataifa, Mary J Blidge.
Onyesho hili ambalo pia limekuwa la kihistoria kwa Mary J Blidge ndani ya Afrika, limefanyika huko Jijini Lagos Nigeria katika hoteli moja maarufu.
Hii ni moja kati ya rekodi nzuri katika historia ya muziki ya Victoria Kimani ambaye muziki wake umeendelea kupokelewa na kukubalika kwa kasi Afrika.
No comments:
Post a Comment