DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, October 30, 2013

Victoria azidi kufunguka



 


Nyota wa muziki anayeiwakilisha vizuri Kenya kupitia sanaa ya muziki kwa sasa, Mwanadada Victoria Kimani, ameendelea kuwapatia watu sababu za kuamini kuwa yupo katika mahusiano ya kimapenzi na msakata kabumbu wa kimataifa Victor Wanyama kutoka Kenya, licha ya wawili hawa kukanusha
swala zima la kuwepo uhusiano wa aina hiyo kati yao.

Swala hili limeibuka baada ya Victoria kuamua kuandika sifa za mwanaume ambaye anaweza kuwa naye katika mtandao, sifa ambazo kwa mujibu wa wachambuzi zinafanana kabisa na zinamuelezea Wanyama vile alivyo.

Maneno aliyoanidika Victoria yanasomeka “A tall, muscular, fine face, black, hard-working, driven, God-fearing gentleman, as kind of man who sweeps me off my feet..” Maneno ambayo pia yanapewa sapoti ya nguvu na ukaribu ambao Victoria na Wanyama wamekuwa nao kwa muda sasa.

No comments: