DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, October 30, 2013

Lemme Know yakamilika


 


Hatimaye kile kichupa kikali kilichobatizwa jina 'Let Me Know' cha msanii mkali wa miondoko ya kughani nchini Tanzania Chin Bees kimetambulisha leo kupitia Ting'a Kali namba moja kwa vijana EATV.

Kichupa hicho ambacho kimeshirikisha wasanii wa kundi la Navy Kenzo Aika & Nahreel, kimefanyiwa kazi na muongozaji mahiri Khalfan chini ya studio ya Home Town huku utayarishaji ukifanywa na Nahreel pamoja na Mr. Thomas.

Video hii tayari imetabiriwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni moja ya toleo ambalo lina nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri na kuleta mapinduzi katika 'industry' ya utayarishaji video za muziki Tanzania.

No comments: