DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, October 29, 2013

Weasel apata mtoto 'mpya'

 


Mpenzi wa msanii wa muziki Weasel kutoka kundi la Goodlyf, Carol Serwadda ambaye makazi yake ya kudumu yapo nchini Norway, ameamua kuasili mtoto wa kiume ambaye ametambulishwa kwa jina Alvin, mtoto ambaye sasa atakuwa ni sehemu ya familia ya msanii huyu mkali Afrika Mashariki.

Hatua hii inakuja wakati inafahamika kuwa Weasel kwa upande wake, tayari ana watoto 7 kutoka mama tofauti, na mtoto huyu mpya wa kuasili kutoka kwa mpenzi wake huyo, atakuwa ni mtoto wa nane katika familia ya msanii huyu.

Tayari Carol alikwishatangaza kuwa hana tatizo lolote na mpenzi wake kuwa na watoto wengi kutoka kwa mama mbalimbali na ndiyo maana amewakubali wote, na sasa mitaa inasuburi kuona ni lini wawili hawa wataamua pia kuwa na mtoto wao wa kibaiolojia katika harakati za kuendelea kukuza familia hii ambayo inavutia hisia za watu wengi.

No comments: