DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Saturday, November 2, 2013

20 PERCENT – “SKENDO HAZINA NAFASI MAISHANI MWANGU”


 





























Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sana na hatimaye hivi karibuni kuibuka na prodyuza wake wa zamani Man Walter na kuudhihirishia umma kuwa wamemaliza tofauti zao, msanii wa muziki wa kizazi kipya Abbas Hamis a.k.a 20 percent amefunguka juu ya kutopenda skendo kwenye maisha yake.

“Mara zote huwa sipendi ile tabia ya kila mtu kusema kuwa bar ya 20% ile pale au ukimtaka twenty nenda baa flani au club flani maana kwa namna flani zinashusha hadhi ya msanii na kuonekana huna makazi zaidi ya sehemu za pombe au zisizo za heshima. Hata hawa underground wanapoingia kwenye hii gemu wajaribu kuchunguza wasanii wenye heshima kwenye hii industry wanapendelea sana kukaa sehemu gani ili kiuzilinda heshima zao na sio kukurupuka tu hata mikataba ya kazi kufanyia kwenye vilabu vya pombe. In short sipendi skendo.” – 20Percent amefunguka.
Msanii huyo ambaye ana historia ya kuwa msanii pekee ndani ya Bongo aliyewahi kunyakua tuzo tano kwa wakati mmoja ndani ya Kilimanjaro Tanzania Music Award kwa sasa ameshaanza kufanya project ndani ya Combination Sound ambayo itaanza kuachiwa mwisho wa mwaka huu au mwakani mwanzoni. Hapo kabla aliwahi kutamba na nyimbo kali zenye ujumbe mzito kwa jamii kama wile Tamaa Mbaya, Money Money, Mama Neema, Ya nini malumbano, n.k.

No comments: