DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Saturday, November 2, 2013

Muthoni DQ kuachia moja moja

Rapper na mjasiriamali mwenye mikakati ya kipekee katika tasnia ya muziki, Muthoni The Drummer Queen, amejipatia sifa kubwa kwa mtindo ambao ameuweka katika kuiachia albam yake mpya inayokwenda kwa jina MDQ, mtindo ambao sio tu utasaidia kumuongezea kipato, bali pia utatoa nafasi kwa mashabiki kusikiliza kwa muda wa kutosha kazi zote ambazo zipo katika albam.

Mtindo huu wa uachiwaji wa albam ya Muthoni ambayo ina jumla ya nyimbo 10, unahusisha kuachiwa kwa nyimbo moja kila mwisho wa wiki, ambapo kila ngoma itakapotoka mashabiki watapata nafasi ya kununua wimbo huu mtandaoni kwa kutuma code ya wimbo huo wa wiki katika namba za simu ambazo watatangaziwa.

Siku ya leo ambayo ni wiki ya tatu kutoka kuanza kutoka kwa ngoma za albam hii, ambapo ngoma ya tatu inayokwenda kwa jina Reconditioned ndiyo inatoka, na sasa zoezi hili litaendelea kwa wiki 7 zaidi mpaka kazi zote zitakapotoka kupitia zoezi hili ambalo limeanza kueleweka na kupokelewa vizuri.

No comments: