DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Monday, November 11, 2013

Akalimu ya Bobi yafana


 
Msanii Bobi Wine ameacha rekodi ya aina yake baada ya kufanya onyesho lake la hisani la Akalimu kwa mafanikio makubwa, na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa mashabiki ambao walileta vitu mbalimbali kama mchango wao kuwasaidia wananchi wenzao walio katika uhitaji zaidi.

Bobi Wine alikata kiu ya mashabiki wake kwa kufanya onyesho kwa saa mbili mfululizo jukwaani, na kivutio kingine kikubwa katika onyesho hilo kilikuwa ni pale Mr G kutoka Jamaica alipopanda jukwaani kuimba live kolabo yake na Bobi Wine inayofahamika kama Swaggerific.

Onyesho hili pia lilipata sapoti ya kutosha kutoka kwa wasanii Jose Chameleone, Gravity Mutujju, Eddie Kenzo na wengineo wengi kutoka kundi maarufu la Fire Base.

No comments: