
Msanii AY ambaye
anafanya vizuri kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye tuzo zinazotarajia
kufanyika hivi karibuni za Channel O, amefanikiwa kuwapiku washiriki
wengine na kupanda kwenye Top 5 ya #TwitterLeague #Choamva baada ya
kuwatupa Radio & Weasel kwenye kinyang’anyiro kinachoendelea ndani
ya chati iyo..
AY anakamata namba 4 sasa kwenye ligi hiyo toka nafasi ya 6 siku ya jana, ambapo Radio na Weasel ndiyo wanashikila nafasi hiyo
Endelea kumtaja AY on Twitter pamoja na kuweka hashtag ya #CHOAMVA
uongelee chochote kumhusu, ili mwakilishi wetu huyu azidi kupanda chati!
Tanzania tunaweza … Na bila kusahau kumpigia kura msanii AY kwa ajili
ya kumwezesha kuibuka mshindi katika tuzo ambazo anaziwania Channel O.
No comments:
Post a Comment