DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, November 8, 2013

Ngoma ya Shaa yanyofolewa


 
Baada ya kuachia video ya ngoma yake maarufu ya Sugua Gaga ambayo imepokelewa vizuri sana hususani katika mtandao wa Youtube, Msanii Shaa amesema kuwa ameshangazwa sana na kustushwa na kitendo cha watu wasiofahamika kuitoa video hiyo katika mtandao kwa madai kuwa audio pamoja na video yake ni mali yao.

Video hii kwa mujibu wa Shaa, ndani ya siku chache ilikuwa imeshajipatia watazamani zaidi ya 45000, ambapo yeye pamoja na timu yake wameshangazwa na kitendo cha video hii kutolewa kwa madai
kuwa haikuwa kazi yao.

Mpaka sasa mwanadada huyu pamoja na timu yake wanafuatilia kuona ni nini chanzo cha hujuma hii kubwa ambayo kiukweli imerudisha nyuma jitihada za kuitangana na kuionyesha kazi hii kwa dunia
kupitia mtandao.

No comments: