DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, November 14, 2013

AY: Tuzo 18 na 'bado'...

 

Msanii wa muziki mwenye mafanikio makubwa Tanzania, AY ameweka wazi kuwa tangu safari yake ya muziki ilipoanza mpaka kufikia leo, ameweza kujinyakulia tuzo za kitaifa na kimataifa 18 sambamba na kutajwa kuwania nyingine mbalimbali.

Msanii huyu ambaye anaiwakilisha poa Tanzania nje ya mipaka yake huku akijivunia mafanikio haya makubwa, amewataka mashabiki wake kuendelea kumuonyesha ushirikiano wa kutosha ili kusaidia kufikisha mbali zaidi harakati zake za kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa kupitia muziki.

AY, hivi sasa anawania tuzo ya Video Bora kutoka Afrika Mashariki pamoja na Video Bora ya msanii wa kiume kutoka kituo kimoja maarufu cha televisheni Afrika na sasa zoezi la kupiga kura bado linaendelea kwa njia ya simu pamoja na mtandao.

No comments: