DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, November 14, 2013

Nas kuinua vipaji UG

 

Rapa mahiri wa hip hop duniani, Nas yupo katika mchakato wa kutengeneza midundo na pia kuongoza filamu inayofahamika kama Shake The Dust ambayo inahusisha wacheza dansi na Ma-rapa wa Hip Hop kutoka nchini Uganda, Colombia, Cambodia pamoja na Yemen.

Filamu hii ina lengo maalum la kuwapatia wasanii hawa chipukizi nafasi ya kuonyesha uwezo wao katika ngazi ya kimataifa, nafasi ambayo itawawezesha kuyafikia malengo na mafanikio katika fani wanayoifanya.

Nas kuhusiana na mpango huu amesema kuwa, kitu ambacho wasanii hawa chipukizi wanakifanya kutoka sehemu hizi mbali mbali duniani zinamkumbusha ni kwanini alitokea kuipenda Hip Hop, na umuhimu wa Hip Hop katika kutumia akili na ubunifu kufikisha ujumbe kwa jamii.

No comments: