DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, November 1, 2013

Bee Man kuzimeki mtandaoni


 

Msanii wa muziki wa hapa Tanzania, Bee Man ambaye anafanya kazi zake za muziki chini la lebo ya Love Child ya huko Nairobi nchini Kenya, ameendelea kupiga hatua katika muziki wake, ambapo safari hii mkali huyu amepata shavu la kusign mkataba na mtandao maarufu wa Mdundo, unaohusika na biashara ya kazi za wasanii mtandaoni.

Bee Man ambaye kwa sasa anafanya poa kwenye airtime na ngoma yake ya Kizunguzungu ambayo amemshirikisha Wyre, amesema kuwa mkataba huu ni moja kati ya fursa nzuri ambayo itasaidia kumuongezea kipato kupitia kazi yake ya muziki.

Msanii huyu amesema kuwa, katika mkataba huu, Ngoma zake kali ikiwepo Embe Dodo pamoja na Kizunguzungu zitaingia katika mtandao huu ambao una wigo mkubwa wa mashabiki na wafuatiliwaji wa kazi nzuri za wasanii, na kadria ambavyo kazi yake itakuwa inapokelewa vizuri na watu, ndivyo atakavyokuwa akijihakikishia kuingiza maburungutu ya pesa kila mwisho wa  mwezi.

No comments: