DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, November 1, 2013

Cannibal kuwarusha watu Dubai

 
Msanii Cannibal anatarajia kufanya onyesho kubwa kabisa huko Uarabuni katika nchi ya Dubai tarehe 8 mwezi Novemba, ndani ya ukumbi maarufu uliopo huko Bur, hatua ambayo ni ishara tosha kuwa nyota ya msanii huyu imeanza kungara nje ya mipaka ya nchi yake.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Cannibal kufanya onyesho huko Dubai ambapo amejipanga kuacha rekodi nzuri kwa shoo ya aina yake,  ambapo mpaka sasa michongo yote ya maandalizi ya onyesho hili imekaa kwenye mstari.

Cannibal ameweza kujipatia umaarufu mkubwa ndani ya Afrika Mashariki hasa kupitia kazi zake alizofanya kama vile Street Hustler, Kichwa Kibov aliyofanya pamoja na Sharama, My City My Town aliyofanya na Prezzo na My Reason aliyomshirikisha Habida

No comments: