
Mkali huyu ambaye ametua hivi karibuni akitokea huko Afrika Kusini, akiwa na nia ya dhati ya kutela mapinduzi katika swala zima la kiwango na utaalam wa video za muziki bongo amesema kuwa ataanza kuingia darasani mwezi wa nne mwaka kesho kujinoa zaidi katika maswala ya motion film pamoja na kutengeneza mahusiano na ma-director wa kimataifa wa videos na pia kupata cheti ambacho kitasaidia kukubalika kwa kazi zake za video hata katika vituo vya kimataifa vya televisheni.
Benjamin amesema kuwa katika kipindi hiki pia atatumia nafasi aliyoipata kuwavuta wasanii wa hapa nyumbani na kufanya nao video za kiwango cha kimataifa huko Afrika Kusini na hivyo kujenga heshima ya video na ma-directors wa hapa nyumbani katika swala zima la viwango vya kazi wanazozitengeneza.
No comments:
Post a Comment