DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, November 13, 2013

Jose, Cindy wazika bifu?

 
Tofauti kubwa ya kimaelewano iliyokuwa inaendelea kati ya msanii Jose Chameleone na Papa Cindy kutoka nchini Uganda, huenda ikawa imefikia kikomo hasa baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa, Chameleone amebadili mtazamo wake na yupo tayari kumrudisha msanii huyu katika familia yake ya Leone Island Crew.

Taarifa hii inaweka wazi pia kuwa, Chameleone pia ameruhusu DJ wake kuendelea kutumia nyimbo ambazo alikuwa amefanya na msanii huyu kama kolabo, na hii ni baada ya kuzisimamisha kwa muda wote ambao walikuwa hawapo vizuri.

Kubadili mawazo kwa msanii huyu kunatajwa kuwa ni baada ya hatua ya mtoto wa Papa Cindy anayefahamika kwa jina Ryan kumfuata Chameleone na kumuomba amsamehe baba yake, kitu ambacho msanii huyu aliguswa nacho na kukitelekeza.

No comments: