
Koko Master maarufu zaidi kama D Banj, Msanii wa muziki ambaye anafanya vizuri kutoka nchini Nigeria, ameripotiwa kutengana na Jennifer Obayuwana, mrembo aliyedumu katika mahusiano naye kwa muda wa miezi 8 sasa.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimetolewa, chanzo cha kufukia kikomo kwa mahusiano haya kimetajwa kuwa ni ratiba kali za wawili hawa, ambapo D Banj amekuwa akibanwa na ziara za muziki wake, wakati Jennifer akiwa bize na biashara zake na za familia yao.
Kuvunjika kwa mahusiano haya kumezima matumaini ya wengi ambao walitarajia kushuhudia harusi ya kihistoria pamoja na kuundwa kwa familia ya aina yake na wawili hawa, hasa kutokana na hadhi na uwezo wa kifedha walionao.
No comments:
Post a Comment