
“When Skelewu meet
Ngololo..Stay tuned..we coming baby..WCB for life hunny” ni maneno ya
Diamond Platnumz aliyoandika kwenye baadhi ya picha alizoshare na
mashabiki wa nyimbo zake muda mfupi uliopita…
Kupitia tovuti ya msanii huyu, This is Diamond, Platnumz ame-share picha za utengenezwaji wa ngoma hiyo ndani ya studio za hit maker wa “Skelewu” , Davido ambazo zinaonyesha na kuelezea kwa ufupi kuwa mambo karibia yanakaa sawa hivyo watu wakae mkao wa kula…

Ni juhudi pamoja na sala ndizo ambazo zinamfanya msanii huyu kuweza kuthubutu na kufanya mambo mazuri zaidi kwenye muziki wa Bongo flava hapa Tanzania…Kupitia collabo hii, Diamond anaendelea kufungua milango kwa muziki wa Tanzania kuskika si Tanzania pekee, bali hata Afrika nzima na Ulimwengu wote kwa ujumla..

Kila la kheri Platnumz katika kulifanikisha hili…
No comments:
Post a Comment