Mashairi yake na mtindo wa uimbaji anaoutumia kwenye ngoma zake
unamfanya awe ni mmoja kati ya wasanii wakali zaidi kwa nyakati hizi
Tanzania.
Uwezo wake kiuimbaji ndo umemfanya achukue tuzo kila mwaka tangu rasmi
kuzitambulisha ngoma zake redioni. Mpaka sasa ameshagonga ngoma kali
nyingi kama vile Nikikupata, Pete n.k na hivi karibuni anatesa na ngoma
yake ya Jikubali.
“Najiamini sana kwamba nina uwezo na namshukuru Mungu hata wasanii
wenzangu wengi wananikubali sana na kunishauri mengi lakini hii hali
hainifanyi mimi kufanya ngoma kila siku japokuwa nina uwezo wa kuachia
ngoma mfululizo.” – Ben Paul.
“Ili thamani yangu iendelee kuwa palepale na kuongezeka zaidi ni
lazima nichukue muda mwingi sana kufikiri nini kinahitajika kwenye soko
la mziki wetu na wenzangu hawafanyi, so hali hii ya uwepo wa artists
wengi wenye uwezo na kiu ya mafanikio si ya kukurupuka na kutoa ngoma
tu. Lazima ufikiri sana ndo ufike pale unapopataka.” – Ben Paul.
Pia alimaliza kwa kusema kuwa kwenye muziki kuna hitaji utulivu
wakati unapotaka kutunga wimbo kwakuwa unaweza ukajikuta una rudia vitu
ambavyo tayari umekwisha vitoa au wenzako wamefanya.
No comments:
Post a Comment