DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, November 6, 2013

Jhiko Man kufanya ziara kubwa


 
Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya reggae nchini Tanzania ambaye hufanya muziki wake kimataifa zaidi,  Jhikolabwino Manyika almaarufu kama Jhikoman, ameweza kupata shavu la nguvu kwa kujiandaa na ziara kubwa ya muziki kimataifa iliyobatizwa jina 'Jhikoman World Tour 2014-2015'.

Jhikoman ambaye anatamaba na nyimbo mbalimbali ikiwemo kichupa chake kipya cha singo 'Bagamoyo' aliyomshirikisha Fid Q na Mzungu Kichaa, kupitia mahojiano yake na eNewz ameweka wazi kuwa ziara hii kubwa itaanza rasmi hapo mwakani ambapo ataanzia katika tamasha kubwa la muziki la Sauti za Busara Zanzibar na kuendelea Sehemu nyingine barani Afrika, Ulaya, Marekani hadi nchini Jamaica.

Mwanamuziki huyo anayetamba na albamu zake kama 'Moyo Unadunda' na 'Yako' amesema ziara yake hii kwake yeye anaitafsiri kama 'Mind Shifting Tour' yaani ziara ya kubadilisha mtazamo.

Jhikoman ameongezea kuwa katika ziara hii pia, mawakala wake waliopo nchini Uingereza, Ufaransa, Finland, Marekani na Ujerumani watamfanyia mpango wa kurekodi na kufanya kazi na wanamuziki mbalimbali kutoka katika nchi hizo.

No comments: