DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, November 7, 2013

Umati wamzika DJ Rankim

 
Rankim Ramadhani Nyamkah maarufu kama DJ Rankim ambaye alifariki jana katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi ya tumbo, amezikwa leo katika makaburi ya Sinza, Jijini Dar es Salaam.

Mbali na ndugu, jamaa na marafiki,  msiba huu umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa muziki pamoja na wasanii ambao kila mmoja kwa nafasi yake ameonyesha kuguswa mno na kifo cha DJ huyo mahiri aliyejizolea sifa kemkem wakati wa uhai wake.

Marehemu DJ Rankim ameacha mtoto mmoja wa kiume pamoja na mke, nasi  eNewz tunaomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi Aamin.

No comments: