DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!
Thursday, November 7, 2013
JOHN WOKA KUIBUKIA KWENYE FILAMU ZA COMEDY
Mwanamuziki mkongwe John Worker ambaye alikuwa anaunda kundi la Wa2ku2 akiwa pamoja na Ras Lion ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na style yake ya uimbaji kama mlevi huku ngoma kama Nieleze ft Keisha zikizidi kumuweka juu kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva.
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu hatimaye BK ilimtafuta ili kuzungumzia sababu za ukimya wake na kufunguka juu ya kubadili kwa muda aina ya sanaa kutoka kwenye mziki hadi kwenye uigizaji na kusisitiza kuwa hajaacha muziki na hafikirii kufanya hivyo.
“Sio kwamba nilikuwa imya kisanii ila niliamua kubadili aina ya sanaa kwa muda ambapo nimekuwa nikifanya maswala ya uigizaji na nimeshafanya muvi nyingi za comedy ambazo si muda mrefu zitaanza kuingia mtaani.” – John Worker.
“Pia ujio wa muvi hizo utaambatana na nyimbo zangu tatu ambazo nitaziachia kwa awamu moja baada ya nyingine. Ngoma hizo ni ‘RAHA UTAMU’, MKORA na ‘NGOMA IKO POA’ ambaye nitamshirikisha Prof. Jay.” – John Worker.
Kwasasa John anaishi pande za Kimara akiwa amepanga na bado hajaanzisha familia yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment