DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, November 7, 2013

Wande adaiwa kuiba wimbo

 

Muandaji muziki na msanii Don Jazzy ameibuka na kumshambulia msanii mwenzake Wande Coal kwa tuhuma kuwa amemuibia wimbo wake unaokwenda kwa jina Baby Face ambao kwa madai yake aliurekodi kama demo mwaka mmoja uliopita.

Don amemshutumu Wande ambaye hapo awali alikuwa akimsimamia kazi zake chini ya lebo yake ya Mavin Records kuwa alichokifanya ni uhalifu mkubwa na ni kumvunjia heshima yake.

Hadi sasa hakuna majibu yoyote kutoka kwa Wande Coal ambaye anatajwa kuachana na D Banj na Mavin Records kwa madai kuwa Don Jazzy hakuwa na mpunga wa kutosha kuwasimamia wasanii ambao walikuwa chini ya lebo hii.

Wimbo huu unaodaiwa kuibiwa umeachiwa na Wande hivi karibuni akiwa chini ya usimamizi wa Black Diamond Entertainment ambayo ndiyo inaendesha kazi zake kwa sasa.

No comments: