
Kundi la muziki ambalo limekuwa gumzo kwa sasa Afrika, Mafikizolo ambalo linaundwa na Theo Kgosinkwe pamoja na Nhlanhla Sibongile Mafu Nciza ambalo limekuwa katika muziki kwa muda mrefu sasa kwa mujibu wa rekodi za mtandaoni, katika kipindi cha mwezi Septemba mpaka sasa, idadi ya mauzo ya kazi zao za zamani pamoja na za hivi karibuni imeongezeka kwa kasi kubwa.
Kundi hili ambalo pia limeingia katika vinyanganyiro vya tuzo mbalimbali za muziki, katika wakati huu ambapo linajivunia mafanikio haya, pia lipo katika mchakato wa kushughulikia albam yake ya 9 baada ya ile ya mwisho inayokwenda kwa jina Reunited iliyotoka mwaka 2012.
Kundi hili limekuwa na historia ya kusisimua pamoja na changamoto mbalimbali katika safari yao ya muziki tangu lilipoanza miaka ya 90, ambapo kwa sasa wamekuwa ni moja kati ya mifano mizuri ya matunda ya kujituma na kuwekeza katika muziki wa kiafrika.
No comments:
Post a Comment